Hukumu ya Mkude SIMBA SC yapigwa kalenda

0
199

Na Abdallah N’ganzi

Kamati ya nidhamu ya SIMBA SC imeahirisha kutoa hukumu kwa mchezaji wao Jonas Mkude kufuatia madai ya kutomalizika kwa ushahidi wa vipimo kwa mchezaji.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Suleiman Kova, imesema kamati imepata fursa ya kusikiliza ushahidi wa upande wa Klabu ya Simba na ushahidi wa mchezaji Jonas Mkude.

Kova amesema baada ya kupokea ushahidi huo, upande wa Jonas Mkude umeeleza kuwa alishindwa kufika mazoezini kutokana na majeraha hivyo Kamati imeruhusu kufanyiwa na Daktari ili kuthibitisha hilo.

Hii si mara ya kwanza kwa mchezaji Jonas Mkude kufikishwa mbele kamati ya nidhamu kutokana na makosa mbalimbali anayoyafanya