Waethiopia 62 wanaswa kwa kuingia nchini kinyemela

0
263

Ofisi ya Uhamiaji mkoani Iringa kwa kushirikiana na Jeshi la polisi mkoani humo, wamewakamata raia 62 wa Ethiopia waliongia nchini kinyume cha taratibu.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa, Juma Bwire amesema raia hao wa Ethiopia wamekamatwa tarehe 3 mwezi huu katika eneo la Ruaha Mbuyuni wilayani kilolo wakiwa wamepakizwa kwenye lori.

Amesema katika lori hilo, Waethiopia hao walifichwa kama mizigo nyuma ya madumu ya mafuta ili wasionekane kirahisi.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la polisi mkoani Iringa linawashikilia raia watatu wa Tanzania ambao ni dereva wa lori hilo, utingo wake psmoja na dalali aliyefanikisha kazi ya kuwasafirisha raia hao 62 wa Ethiopia.