Kuuza dawa na vipodozi kwenye mabasi ni kinyume na sheria.

0
372

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tazania (TMDA) imesema kufanyabiashara ya dawa na vipodozi kwenye mabasi ni kosa kisheria.

Akizungumza katika kikao kazi kati ya TMDA na waandishi wa habari wa mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro kilichofanyika jijini Arusha, Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Dawa na Vifaa Tiba, Dkt. Yonah Mwalwisi amesema sheria za udhibiti wa dawa na vifaa tiba hairuhusu uuzwaji holela wa dawa na watakaokutwa na hatia ya kufanya kosa hilo faini yake si chini ya shilingi laki 1.

Mwalisi amesema sheria haziruhusu kufanyika kwa matangazo ya dawa ndio maana huwezi kukuta hospitali au maduka ya dawa yakitangaza dawa zilizopo katika maeneo yao.

Aidha, amewaomba wananchi kutoa taarifa kwa TMDA pale wanapobaini kukiukwa kwa sheria za dawa na vifaa tiba ikiwemo uduni wa bidhaa na utupaji holela wa vifaa tiba vilivyotumika ikiwemo mipira ya kondomu.