Figgers: Milionea aliyetelekezwa akiwa kichanga

0
202

Akiwa na miaka nane, Mhandisi na mmiliki wa “Figgers Communications”, Freddie Figgers aliamua kumuuliza baba yake kuhusu alivyozaliwa. Majibu ya swali hili yalimfanya Freddie ajisikie vibaya na kujihisi kama takataka.

Mwaka 1989 Nathan Figgers fundi na mkewe ambaye alikuwa mkulima wakiwa kwenye miaka ya 50 waliokota mtoto kando ya pipa la taka akiwa na siku mbili.

Wawili hao hawakutaka kumtoa mtoto huyo katika kituo cha watoto yatima hivyo kumchukua kama wao na kumlea mtoto huyo hadi alipofikia.

Freddie Figgers (31) ni mbunifu na mbobezi wa masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambaye hadi mwaka 2020 kampuni yake inayojihusisha na utengenezaji wa simu za ‘Figgers,’ vifaa vya afya vinavyotumia TEHAMA na mambo mengine mengi ndiyo kampuni pekee ya mawasiliano ‘telecom’ inayomilikiwa na mtu mweusi huko Marekani.

Kazi yake imempa umaarufu na kumuweka kwenye chati ya mamilionea akiwa bado na umri mdogo.