Sakho kuwekeza soka la vijana Zanzibar

0
179

Mwanasoka wa Ufaransa, -Mamadou Sakho Mamadou ambaye yuko ziarani huko Zanzibar, amefanya mazungumzo na maofisa wa wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na wa wizara ya Utalii na Mambo ya Kale zote za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Miongoni mwa mambo yaliyozungumzwa katika kikao hicho ni unzishwaji wa kituo cha kufundishia soka kwa vijana na namna ya kuutangaza utalii wa Zanzibar.

Awali, Mamadou akiwa na mkewe alikutana na kufanha mazungumzo na Rais wa ZanzIbar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi Ikulu jijini Zanzibar, ambapo alimkabidhi mwanasoka huyo zawadi ya mlango wa ZanzIbar kama ishara ya kivutio cha utalii.

Rais, Dkt. Mwinyi pia alimkabidhi zawadi ya viungo mke wa mwanasoka huyo ikiwa ni ishara ya kivutio cha utalii wa Zanzibar.

Sakho ambaye ni Balozi wa asasi za kiraia duniani, ameamua kuitangaza Tanzania kimataifa kwa kuwa balozi wa hiari wa utalii wa Zanzibar.

#utaliiwandani #Tanzaniaunforgettable #utaliizanzibar #SakhoTanzania