Nay wa Mitego atoka hospitali

0
1448

Msanii wa Bongo Fleva Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupata matibabu kufuatia ajali ya pikipiki aliyoipata jana usiku akielekea kwenye mahojiano na kipindi cha ‘Empire’ cha E-FM.

Akizungumza na TBC, Meneja wa Nay, Masudi Kandoro ‘Meneja Kandoro’ amesema msanii huyo amepata ajali ya bodaboda wakati akiwahi kwenye mahojiano hayo.

“Alikuwa na Interview [mahojiano], kipindi cha Empire cha E-FM, kwa hiyo jana kidogo kulikuwa na foleni wakati anaelekea huko kwa hiyo alivyofika kwenye mazingira ya Kawe, akaona foleni ni kubwa, akaamua achukue bodaboda, kwa sababu ya ule uharaka bodaboda akagonga gari,” amesema Kandoro.

Meneja Kandoro amesema si kawaida Nay wa Mitego utumia Bodaboda kwani ana usafiri wake, ila kutokana na mazingira aliyokutana nayo akaamua kupanda bodaboda.

“Nay sio mtu wa bodaboda ila kwa sababu ya uharaka na umuhimu wa interview akaona achukue bodaboda ili aweze kuiwahi foleni,”ameongeza Kandoro.