Kampuni zaagizwa kuzalisha mbegu nchini

0
222

Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ameziagiza kampuni zote zinazonunua mbegu nje ya nchi kuanza kuzalisha hapa nchini, lengo likiwa ni kukuza sekta ya Kilimo.

Dkt. Mpango ametaka ukuaji wa teknolojia uendane na uzalishaji wenye tija katika sekta ya Kilimo, na ameiagiza wizara ya Kilimo kusimamia uzalishaji wa mbegu bora nchini.

Dkt. Mpango ametoa agizo kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mkoani Morogoro wakati wa mdahalo wa Kumbukizi ya Hayati Edward Moringe Sokoine aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania.

“Nataka kampuni zote zinazoagiza mbegu nje ya nchi zizalishe hapa hapa nchini, na msinisubiri kuwauliza.”, amesema Dkt. Mpango.

Dkt. Mpango amesema hatua ya kampuni mbalimbali kuzalisha mbegu bora za kilimo hapa nchini itasaidia kupunguza utegemezi nje ya nchi pamoja na kufanya kilimo chenye tija.