Wakulima wahakikishiwa uhakika wa soko

0
189

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kusimamia bei za mazao na kuhakikisha Wakulima wanakuwa na soko la uhakika la mazao yao.
 
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kyerwa, – Innocent Bilakwate katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, ambapo mbunge huyo alitaka kufahamu mpango wa Serikali wa kuhakikisha zao la Kahawa linakuwa na soko la uhakika.
 
“Kahawa ni miongoni mwa mazao ya kimkakati ambayo yanalimwa na jamii pana, hivyo Serikali itaendelea kusimamia ushirika na masoko ili wakulima waweze kulipwa kwa wakati,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
 
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa pamoja na kutatua changamoto ya masoko, Serikali pia imeendelea kutekeleza mkakati wa uanzishwaji wa viwanda ndani ya nchi ili zao la kahawa liweze kuongezewa thamani na kuwa na soko la uhakika.