Rais: Maafisa habari toeni taarifa za Serikali

0
321
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam Mei 7, 2021 katika Mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Mlimani City mkoani Dar es Salaam.

Rais Samia Suluhu Hassan amewataka maafisa habari nchini kuendelea kuhimizana kuhusu utoaji taarifa kwa umma, huku wakizingatia namna bora ya kuwasilisha taarifa hizo.

Akisoma ujumbe mfupi (sms) wa Rais Samia Suluhu Hassan katika kikao cha 14 cha maafisa habari, mawasiliano na uhusiano kinachofanyika jijini Mbeya, Katibu Mkuu wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema Rais amewataka maafisa hao wasiache yale yanayolalamikiwa na jamii kuendelea, kabla ya kutolewa ufafanuzi.

Awali akizungumza katika hicho, Waziri wa Habari, Innocent Bashungwa amesema wataendelea kuboresha mawasiliano serikali kwa kuhakikisha maafisa habari wa wizara pamoja na TAMISEMI wanafanya kazi kwa ushirikiano na kuwafikia wananchi kwa wakati .