TEF yalaani Wanahabari kudhalilishwa

0
277

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limelaani vitendo vya baadhi ya Polisi na Watendaji wa Serikali kuwapiga, kuwadhalilisha na kuharibu vifaa vya kazi vya Waandishi wa Habari wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao, na kuongeza kuwa vitendo hivyo havikubaliki.

Akizungumza mjini Morogoro wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa Wahariri wa Habari nchini na Kongamano la Kitaaluma, Kaimu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile amesema kuwa Waandishi wa Habari ni jicho la jamii na kwamba kama kiongozi anafanya jambo jema hapaswi kuhofia uwepo wa Waandishi wa Habari.