Waziri Mwambe kushughulikia wawekezaji waliokwamishwa

0
288

Waziri wa uwekezaji Geoffrey Mwambe ametoa siku 14 kwa wawekezaji wote waliokuwa wamekwamishwa kuwekeza na Taasisi za serikali kuandika barua ya kueleza namna walivyokwamishwa ili waendelee na mchakato wa kuomba kufanya uwekezaji hapa nchini

Waziri Mwambe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kukutana na wafanya wa kituo cha uwekezaji TIC ili kuangalia namna ya kuboresha shughuli za uwekezaji kwa wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi

Aidha amesema kuwa kila muwekezaji anapaswa kupitia TIC maana ndio chombo mahususi kwa kusimamia shughuli zote za uwekezaji hapa nchini na kuwa hakuna muwekezaji ataomba kuwekeza nchini atazuiliwa endapo atakidhi vigezo na masharti ya kuwekeza hapa nchini.

Waziri Mwambe amesema kulikuwa na vikwazo mbalimbali ikiwepo kwa wawekezaji ambapo amesema serikali ejipanga kukabiliana na changamoto hizo ili kuwawezesha wawekezaji waliokuwa tayari kuwekeza hapa nchini

“Niwaambie tu kuwa wawekezaji wa ndani na nje ya Nchi wanaotaka kuwekeza Hapa nchini kuwa serikali imejipanga kubaliana na vikwazo vyote vilivyosababisha Baadhi ya wawekezaji kushindwa kuwekeza Hapa Tanzania maana lengo letu ni kupata wawekezaji wengi zaidi” Ameeleza Waziri Mwambe

Hata hivyo Waziri Mwambe amesisitiza uadilifu na uwajibikaji kwa watendaji wanaohusika kutoa huduma kwa wawekezaji ili kuwa na weledi katika kuwahudumia wawekezaji Hapa nchini.