Wanamgambo wa Taliban wa nchini Afghanistan wamekana kuhusika na milipuko iliyotokea nje ya shule moja ya sekondari ilyopo katika mji mkuu wa nchi hiyo Kabul, na kusababisha vifo vya takribani Wanafunzi sitini.
Wanamgambo hao wamekanusha shutuma hizo kufuatia taarifa iliyotolewa na maafisa wa Serikali ya Afghanistan iliyodai Wanamgambo hao kuhusika na milipuko hiyo iliyotokea kwenye eneo la Dasht-E-Barchi.
Habari zaidi kutoka nchini Afghanistan zinaeleza kuwa, mazishi ya Wanafunzi waliofariki dunia katika milipuko hiyo yanaendelea katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.
Mpaka sasa hakuna kikundi chochote kilichodai kuhusika na milipuko hiyo na kwamba Serikali ya Afghanistan imewataja Wanamgambo wa Taliban kwa kuwa wamekuwa wakihusika na matukio mengi kama hayo katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo.