Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa madini GST imewataka wachimbaji wadogo wa madini mkoani Singida kuyatumia mafunzo yanayoendelea kutolewa na taasisi hiyo mkoani humo kuboresha shughuli zao za uchimbaji.
Akizungumza na wachimbaji Hao katika mgodi wa madini wa Sekenke One mkoani Singida, Mjiolojia kutoka GST Charles Moye amesema mafunzo hayo yamemlenga moja Kwa moja mchimbaji mdogo ili kumuinua kiuchumi kupitia sekta ya madini.
Nao wananchi mbalimbali waliofikiwa na mafunzo hayo hadi Sasa wameishukuru taasisi ya GST Kwa uamuzi wa kutoa mafunzo Kwa wachimbaji wadogo mkoani Singida na kuyataka mafunzo hayo kuwa endelevu ili kuwafikia wachimbaji wengi zaidi wanaokabiliwa na changamoto katika uchukuaji wa sampuli za udongo ili kubaini eneo sahihi linalofaa Kwa uchimbaji.
Mafunzo hayo tayari yameshatolewa Kwa wachimbaji wa madini mkoani Dodoma, na Sasa yapo Singida ambapo wiki ijayo yanatarajiwa kutolewa Kwa wachimbaji mkoani Tanga.