Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa taarifa kuhusu kilichotokea jana katika uwanja wa Benjamin Mkapa na kupelekea mechi Kati ya Simba dhidi ya Yanga.
Shirikisho hilo imeomba radhi wadau wote waliolipa viingilio kuingia uwanjani, waliokuwa wakisubiri kuangalia kwenye televishen, kusikiliza redioni na watoa huduma mbalimbali.
Kwa hali hiyo TFF imetoa maelekezo kwa bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kutoa taarifa za kina kuhusu kuahirishwa kwa mchezo huo, pamoja na kushughulikia hatma ya wapenzi wa mpira wa miguu waliolipa viingilio kuingia uwanjani.