Jeshi la Polisi laanza kutekeleza agizo la Rais

0
405

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro, ametoa muda wa mwezi mmoja kwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kuhakikisha linakomesha vitendo vya uhalifu mkoani Dar es salaam.

IGP Sirro ametoa agizo hilo, ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa hapo jana wakati wa mkutano wake na Wazee wa mkoa wa Dar es salaam, ambapo alimtaka kuhakikishwa vitendo vya uhalifu ambavyo vimeendelea kushamiri katika maeneo mbalimbali nchini vinakomeshwa mara moja.

Amewataka Wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi Nchini, na kwa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa amewaagiza kuanzisha vikundi vya ulinzi shirikishi vitakavyosaidia kukomesha vitendo ya uhalifu.

Aidha, IGP Sirro amewataka watu wote wanaopata msamaha wa vifungo kutoka gerezani kuacha kujihusisha na vitendo vya uhalifu na uvunjifu wa amani, na wakiendelea na vitendo hivyo Jeshi la Polisi litaendelea kutumia sheria zilizopo ili kuwashughulikia.