Wafanyabiashara machinjio ya Vingunguti watakiwa kuzingatia usafi

0
276

Msajili wa Bodi ya Nyama Nchini Dkt. Daniel Mushi amewataka Wafanyabiashara wa nyama wanaofanya shughuli zao katika machinjio ya Vingunguti mkoani Dar es salaam kuzingatia sheria wakati wanapofanya shughuli zao.

Dkt. Mushi ametoa kauli hiyo alfajiri ya leo alipotembelea machinjio hayo, kwa lengo la kukagua  shughuli zinazoendelea.

Akiwa machinjioni hapo, Dkt. Mushi amesema ni ukweli kwamba miundombinu ya machinjio hayo ni duni na imezidiwa uwezo,  jambo ambalo Serikali imeshaliona na ndio maana imejenga machinjio mapya na ya kisasa.

Kwa mujibu wa Dkt. Mushi, uwezo wa machinjio hayo ya Vingunguti ni kuchinja ng’ombe 20 kwa siku, lakini wanachinja ng’ombe 400 na wakati mwingine wa sikukuu wanachinja mpaka ng’ombe 1, 000 na hivyo kufanya usimamizi kuwa mgumu.

Naye Afisa Mfawidhi wa machinjio ya Vingunguti, Jabin Yabise amewakumbusha Wafanyabiashara katika eneo hilo.kuendelea kuzingatia usafi ili kulinda afya za walaji.

Ziara hiyo ya Msajili wa Bodi ya Nyama Nchini Dkt. Daniel Mushi ni ya kwanza katika machinjioni hayo ya Vingunguti tangu alipoteuliwa kushika wadhifa huo Aprili Mosi mwaka huu.