Uteuzi wa viongozi watatu watenguliwa

0
256

Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi watatu kuanzia Aprili 30 mwaka huu.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga imeeleza kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Profesa Tadeo Satta.

Sambamba na hatua hiyo, Rais Samia Suluhu Hassan  ametengua uteuzi wa wajumbe sita  wa bodi ya TASAC.

Uteuzi mwingine uliotenguliwa ni wa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, – Hassan Mwang’ombe.

Rais Samia Suluhu Hassan pia ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania Dkt. Harun Kondo.

Sambamba na hatua hiyo, amevunja Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania.

Uteuzi wa viongozi watakaoshika nyadhifa hizo utafanywa baadaye.