Sala ya Eid kitaifa kufanyika Dar es salaam

0
164

Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam Alhad Mussa Salum amesema sala ya Eid El Fitr Kitaifa mwaka inatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja mkoani Dar es salaam

Sheikh Alhad ameyasema hayo mkoani Dar es salaam alipokuwa akitoa salamu kwa Waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa mashindano ya Kimataifa ya Quran Tukufu.

Amesema sala ya Eid itafuatiwa na Baraza la Eid, ambapo Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Sikukuu ya Eid El Fitr inafanyika baada ya kukamilika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, ambao ni nguzo ya tano ya dini ya Kiislamu.