Watumishi wa Serikali na wale wa mashirika ya umma wanaoshiriki michezo ya Mei Mosi kitaifa jijini Mwanza, wametoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wanaoishi katika vituo vya kulea watoto vilivyopo jijini humo.
Mwenyekiti wa kamati ya michezo ya Mei Mosi kitaifa Stanslaus Matimo amesema kuwa, wameamua kutoa msaada kwa watoto hao, ili nao wajione ni sawa na watoto wengine.
Msaada uliotolewa kwa watoto hao ni pamoja na mchele, unga, mafuta, sukari, chumvi, sabuni, magodoro na shuka.
Mbali na kutoa msaada huo, Kamati hiyo ya michezo ya Mei Mosi kitaifa pia imepanga
kugharamia Bima za afya kwa watoto 18 wanaolelewa kwenye vituo hivyo ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.