Rais Samia Suluhu Hassan: JPM ameondoka mwenyewe

0
310

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Serikali anayoiongoza haitakubali kuona rasilimali za Taifa zinachezewa.

Akihutubia Bunge jijini Dodoma, Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa wanaodhani mapambano yaliyokuwa yakifanywa na aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt. John Magufuli yamemalizika baada ya kifo chake wanajidanganya.

Amesema aliyeondoka ni Dkt. John Magufuli lakini mambo yake yote aliyoyapigania hayajaondoka.

Amesema amelazimika kutoa kauli hiyo kutokana na baadhi ya watu kudhani kuwa baada ya kifo cha Dkt. Magufuli watakuwa wanafanya mambo wanavyotaka.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa, kuna baadhi ya mashirika ya umma yameanza kulegalega katika utendaji na Wawekezaji kadhaa waliokuwa katika mazungumzo na Serikali wameanza kurudi nyuma katika mazungumzo hayo.

Viongozi mbalimbali Wastaafu wamefika Bungeni hii leo kwa ajili ya kusikiliza hotuba hiyo ya Rais Samia.Suluhu Hassan Bungeni.

Miongoni mwao ni Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Mzee Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,- Amani Abeid Karume pamoja na Mjane wa Baba Taifa, – Mama Maria Nyerere.