Shilole afunga ndoa ya pili

0
168

Mwigizaji ambaye pia ni Msanii wa Bongofleva wa hapa nchini Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole ama ‘Shishi baby’, amefunga ndoa na Mchumba wake Rajab Issa ‘Rommy’.

Taarifa za Shilole kufunga ndoa na mchumba wake huyo zimejulikana kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Instagram.

Hii inakuwa ndoa yake ya pili rasmi baada ya ile ya kwanza aliyofunga na Ashraf Uchebe kuvunjika.

Baada ya kuweka picha za ndoa yao, Shilole ameandika “Namshukuru Mungu, tumemaliza salama, kwa sasa unaweza kuniita Mrs Rajabu Issa (Rommy)”.