Waziri Ummy amsimamisha kazi Mkurugenzi wa Buhigwe

0
273

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Ummy Mwalimu amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, Anosta Nyamoga kupisha uchunguzi dhidi yake.

Waziri Ummy amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko na tuhuma za ubadhirifu wa fedha na usimamizi usioridhisha wa miradi ya maendeleo katika halmashauri hiyo.

Kutokana na tuhuma hizo Waziri Ummy amemwagiza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI kupeleka timu ya uchunguzi mara moja, na kumwelekeza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuhakikisha timu hiyo ya uchunguzi inapata ushirikiano katika kipindi ambacho itafanya kazi.