TIgo na Zantel zauzwa kwa Axian Group

0
155

Kampuni ya Millicom International inayomiliki hisa katika kampuni za simu za mkononi za Tigo na Zantel, imepanga kuziuza kampuni hizo kwa ubia utakaoongozwa na kampuni ya mawasiliano ya Axian Group yenye makao makuu yake jijini Antananarivo nchini Madagascar.

Kwa muda mrefu kampuni hiyo ya Axian Group imekuwa ikitoa huduma zake katika visiwa vilivyopo kwenye Bahari ya Hindi kwa upande wa Bara la Afrika pamoja na baadhi ya nchi za Ulaya.

Kwa sasa kampuni ya Axian Group inatoa huduma zake kwenye nchi za Madagascar, Senegal, Togo, visiwa vya Reunion na Mayotte pamoja na Comoro.

Kufuatia hatua hiyo, kampuni ya simu za mkononi ya Tigo imewahakikishia wateja wake na umma kwa ujumla kuwa hakutakuwa na mabadiliko yoyote katika utoaji huduma na bidhaa zake na kwamba huduma zitaendelea kama kawaida.

Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo ilianza kutoa huduma zake nchini mwaka 1995.