Mkataba wa ujenzi wa bomba la mafuta watiwa saini

0
228

Rais Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa mkataba kati ya Serikali ya Uganda na kampuni ya Mafuta Ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP) juu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Chongoleani mkoani Tanga.

Katika mradi huo wa ujenzi wa bomba la mafuta, kampuni ya Total ya nchini Ufaransa na ile ya CNOOC kutoka nchini China ni wabia.

Akihutubia katika hafla hiyo ya utiaji saini mkataba huo iliyofanyika Ikulu mjini Entebbe, Rais Samia Suluhu Hassan amesema, mradi huo una manufaa makubwa ya kijamii, kiuchumi na kibiashara kwa Wananchi wa Tanzania na Uganda.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema, mradi huo utaamsha uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na kufungua milango ya biashara ya mafuta baina ya nchi hizo.

Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka bandari ya Tanga utafanyika ndani ya kipindi cha miaka 3.

Rais Samia Suluhu Hassan ameshuhudia utiaji saini wa mkataba kati ya Serikali ya Uganda na kampuni ya Mafuta Ghafi ya Afrika Mashariki (EACOP) juu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda kwenda Chongoleani mkoani Tanga.

Katika mradi huo wa ujenzi wa bomba la mafuta, kampuni ya Total ya nchini Ufaransa na ile ya CNOOC kutoka nchini China ni wabia.

Akihutubia katika hafla hiyo ya utiaji saini mkataba huo iliyofanyika Ikulu mjini Entebbe, Rais Samia Suluhu Hassan amesema, mradi huo una manufaa makubwa ya kijamii, kiuchumi na kibiashara kwa Wananchi wa Tanzania na Uganda.

Rais Samia Suluhu Hassan amesema, mradi huo utaamsha uwekezaji katika ukanda wa Afrika Mashariki na kufungua milango ya biashara ya mafuta baina ya nchi hizo.

Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka bandari ya Tanga utafanyika ndani ya kipindi cha miaka 3 mpaka kukamilika kwake.