Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi kupisha uchunguzi wa madai ya matumizi mabaya ya fedha na rasilimali katika ofisi yake.
Waziri Dkt.Ndumbaro ametoa uamuzi huo leo mkoani Dar es salaam ambapo amesema uchunguzi huo hauhusiani na ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Amesema kwa sasa nafasi ya Mdachi itakaimiwa na Betrita James ambaye ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).