Rais Dkt. Mwinyi awasili Maputo

0
328

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Mwinyi tayari yupo nchini Msumbiji, kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Malavane, Maputo, Rais Dkt. Mwinyi amepokelewa na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo pamoja na gwaride rasmi lililoandaliwa kwa ajili yake.

Mkutano huo wa siku moja unawahusisha wakuu wa nchi wanachama wa SADC na miongoni mwa mambo yatakayojadiliwa ni masuala ya usalama na hatua za kukabiliana na vitendo vya ugaidi katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo.