Rais Samia Suluhu Hassan awasili Zanzibar

0
230

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo amewasili Zanzibar akitokea jijini Dar es salaam, ambapo hapo kesho atahudhuria kumbukumbu ya kifo cha aliyewahi kuwa Rais wa Zanzibar Abeid Amani Karume (Karume Day), itakayofanyika katika Ofisi Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume, Rais Samia Suluhu Hassan amepokelewa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla.

Akiwa Zanzibar, Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi.