JK atoa tahadhari akaunti feki

0
351

Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete ametahadharisha kuhusu uwepo wa akaunti feki inayotumia jina lake katika mtandao wa kijamii wa Twitter.

Kupitia akaunti yake rasmi ya Twitter Dkt. Kikwete amesema akaunti inayotumia jina la Kikwete Mrisho si ya kwake na kuwaomba watumiaji wa mtandao kuipuuza.

Hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la akaunti feki mitandaoni, hali inayowalazimu Wananchi kuchukua tahadhari ikiwemo kuthibitisha mtumiaji wa akaunti husika kabla ya kusambaza ujumbe.