Raia wa China akamatwa kwa kuchapa wafanyakazi

0
151

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia raia wa China, Xiao Yong kwa tuhuma za kuwachapa viboko wafanyakazi wawili wa Kampuni ya Bonanza kwa madai ya kuiba shilingi laki 2.

Akizungumza na wandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya. Urlich Matei amesema wamefanikiwa kumkamata mtuhimiwa mara baada ya kusambaa  video kwenye mitandao ya kijamii ikionesha raia huyo akiwaadhibu wafanyakazi hao kinyume cha sheria.

Aidha, Kamanda Matei ametoa rai kwa wananchi wa mkoa wa Mbeya kuendelea kutoa taarifa za unyanyasaji zinazofanywa na  raia wa kigeni nchini.