Dkt. Mpango: Najua kiatu cha umasikini kinavyouma

0
263

Makamu wa Rais Mteule, Dkt. Philip Mpango ameahidi kufanya kazi kubwa ili kuwahudumia wananchi wa Tanzania ambao wengi wanaishi katika hali ya masikini.

Akiongea mara baada jina lake kutajwa kama Makamu wa Rais Mteule, Dkt. Mpango amesema, akithibitishwa kuwa makamu wa Rais basi kazi yake kubwa ni kumsaidia Rais kuwahudumia wanyonge.

Dkt. Mpango amesema huu ni wakati wa kufanya kazi na kuipeleka Tanzania katika uchumi wa juu na kuwawezesha wananchi hasa masikini kuwa na maisha bora.

Hata hivyo kiongozi huyo mteule ameahidi kusimamia rasilimali za Tanzania kwa nguvu zote ili ziendelee kuwanufaisha Watanzania kwani katika zama hizi hakuna mjomba wa kukuletea kitu.

Jina la makamu huyo litapigiwa kura na wabunge na kuthibitishwa walau na asilimia 50 ya kura za wabunge wote.