Waziri Jafo aanza kuchukua hatua baada ya maelekezo ya Rais

0
279

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo, amemuagiza Katibu Mkuu wa ofisi hiyo Mhandisi Joseph Nyamhanga kuwachukulia hatua Wahazini na Wakaguzi wote wa ndani wa halmashauri zilizopata hati chafu katika ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyowasilishwa leo kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Waziri Jafo ametoa agizo hilo saa chache baada ya kuwasilishwa kwa taarifa hiyo ya CAG Ikulu Chamwino mkoani Dodoma.

Pamoja na mambo.mengne taarifa hiyo imebaini uwepo wa matumizi mabaya ya fedha za Serikali katika baadhi ya halmashauri nchini.

Akitoa maagizo baada ya kupokea taarifa hiyo ya CAG, Rais Samia amemuagiza Waziri Jafo kuhakikisha anasimamia.matumizi.ya fedha za Serikali katika halmashauri, na endapo atashindwa aombe msaada.