Wanajeshi wa Afrika Mashariki wamlilia Magufuli

0
268

Wanajeshi wa Jumuiya ya Afrika mashariki wamlilia hayati magufuli na kuahidi kumuenzi kwa vitendo kwa yale yote aliyoyafanya wakati wote wa uhai wake.

Akiongea mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ofisi ya mkuu wa mkoa Arusha kwa niaba ya majeshi ya nchi sita za Jumuiya ya Afrika Mashariki, mwenyekiti wa majeshi hayo Kanali Rafael Kiptoo amesema, “Tumeshtushwa sana na kifo cha aliyekuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania, Hayati Dkt. John Magufuli”.

Amesema kuwa wao kama wawakilishi wa majeshi ya nchi sita wanamuona Hayati Magufuli kama kielelezo cha kiongozi mzalendo na mbeba maono hivyo wao wataendeleza yale yote aliyowaelekeza wakati wote wa uhai wake.

“Hayati Dkt. Magufuli alikuwa shujaa na kielelezo cha kuigwa mfano, sisi kama majeshi tutamuenzi kwa vitendo katika kuwatumikia wananchi ndani ya jumuiya yetu,” amesema Kanali Kiptoo.

Amewataka wananchi ndani ya Jumuiya ya Afirika Mashariki kuwa na subra na utulivu katika kipindi chote cha maombolezo ya shujaa wetu na mwana wa Afrika na mpigania umoja na mshikamano ndani ya Afrika Mashariki.