Kwaheri Dar es salaam

0
231

Shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli imekamilika kwa mkoa wa Dar es salaam na mwili huo unasafirishwa kuelekea mkoani Dodoma.

Uwanja wa Uhuru ndio uliotumika kwa shughuli hiyo ambayo imefanyika kwa muda wa siku mbili.

Kabla mwili wa Dkt Magufuli kuondolewa katika uwanja huo wa Uhuru kwenda uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, gari lililobeba mwili wa Dkt Magufuli lilizunguka mara tano katika uwanja huo, ili kutoa nafasi mwili huo kuagwa na Wakazi wa Dar es salaam ambao hawakuweza kuaga.

Shughuli hiyo ya kuaga mwili wa Dkt Magufuli ililazimika kukatishwa kabla ya muda uliopangwa, baada ya kubainika kuwa hata likiendelea waombolezaji wote waliokuwepo uwanjani hapo hawataweza kuaga.