Zaidi ya Marais 10 kumuaga Dkt Magufuli Dodoma

0
274

Zaidi ya Marais 10 kutoka nchi mbalimbali, wanatarajiwa kushiriki katika shughuli ya Kitaifa ya kumuaga aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli, itakayofanyika hapo kesho katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt Hassan Abbasi imeeleza kuwa, orodha ya majina ya Marais hao pamoja na ya Wakuu wengine wa Serikali na Wawakilishi wa Mashirika mbalimbali watakaohudhuria shughuli hiyo itatolewa hapo baadaye.

Baada ya kukamilika kwa shughuli hiyo ya Kitaifa ya kuaga mwili wa Dkt Magufuli jijini Dodoma, mwili huo utasafirishwa kwenda Zanzibar ambapo wakazi wa huko nao watapata nfasi ya kuaga.