Dkt. Ndugulile atembelea studio za TBC Arusha

0
192

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari,Dkt. Faustine Ndugulile,amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Shirika la Utangazaji nchini (TBC) katika kutekeleza miradi mbali mbali kupitia taasisi zake ili kuhakikisha kunakuwa na usikivu mzuri wa redio hasa katika maeneo ya mipakani.


Dkt Ndugulile amezungumza hayo alipotembelea studio za Redio ya Jamii TBC ARUSHA ambazo zimefanyiwa ukarabati na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote UCSAF,amesema lengo ni kuhakiiisha Wananchi wanapata usikivu wa kutosha.


Mkurugenzi wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote-UCSAF,JUSTINA MASHIBA,amesema mfuko kwa jushurikiana na Shirika la Utangazaji TBC waliweza kufanya ukarabati wa majengo na studio za kisasa  na wataendelea kushirikiana .


Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini TBC,Happynes Ngasala,amesema ukarabati huo wa majengo na studio umesaidia kuwafikia wananchi.