AstraZeneca yaendelewa kutiliwa shaka

0
290

Uholanzi imetangaza kusitisha matumizi ya chanjo dhidi ya virusi vya corona aina ya Oxford AstraZeneca, kufuatia hofu kwamba chanjo hiyo inaweza kuwa na madhara.
 
Uholanzi imesitisha matumizi ya chanjo hiyo baada ya nchi za Ireland, Denmark, Norway, Bulgaria, Iceland na Thailand kusitisha matumizi ya chanjo hiyo inayodaiwa kusababisha damu kuganda.
 
Hata hivyo Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema hakuna dalili za kuwepo kwa uhusiano kati ya chanjo hiyo na damu kuganda.