Sanduku lenye chatu latelekezwa na kuzua taharuki

0
539

 
Watu wasiofahamika wametelekeza  sanduku lenye nyoka mkubwa aina ya Chatu katika  kata  ya  Isyese Sokoni jijini  Mbeya,  na kuzua  taharuki  kwa  wakazi  wa  eneo  hilo.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa, sanduku lililokuwa na nyoka huyo limetelekezwa majira ya usiku.

Nao baadhi ya wakazi wa kata hiyo ya Isyese Sokoni wamesema kwa muda mrefu hawajawahi kushuhudia tukio kama hilo katika eneo lao,  na hivyo kuomba mamlaka husika kuchunguza tukio hilo ili waondokane na hofu iliyowapata.

Tayari nyoka huyo amechukuliwa na maafisa wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na kwenda kuhifadhiwa.