Corona yaendelea kuitesa Brazil

0
162

Brazil imeendelea kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliofariki dunia baada ya kuugua corona, huku pia maambukizi yakizidi kuongezeka siku hadi siku.

Katika kipindi cha saa 24 zilizopita, watu elfu mbili wamethibitika kufariki dunia baada ya kugua corona nchini humo na wengine zaidi ya laki mbili na elfu 70 wakithibitika kuambukizwa.

Hospitali nyingi nchini Brazil zimetangaza kulemewa na wagonjwa,  wahudumu wameendelea kuwa wachache na vifaa tiba vikiendelea kupungua.