Makamu wa Rais awafunda wanawake

0
269

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka wanawakee kuungana kwa pamoja ili kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo.

Akihutubia katika maadhimisho ya
Siku ya Wanawake Duniani ambayo kwa mkoa wa Dar es Salaam yamefanyika Mlimani City, Mama Samia amewaasa wanawake kuuungana na kuanzisha miradi mbalimbali ili kujiletea maendeleo.

Amesema, ifike wakati kwa wanawake wamiliki njia za uchumi ikiwa ni pamoja na kuanzisha makampuni yao wenyewe.

Kuhusu ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi, Mama Samia amesema kwa sasa hali ni nzuri hasa kwenye vyombo vya maamuzi na nyanya za Siasa.

Ametoa wito kwa taasisi binafsi kuhakikisha zinatoa fursa kwa wanawake katika kusimamia na kuongoza taasisi hizo.