Ulega atoa somo kwa Halmashauri nchini

0
217

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Abdallah Ulega amezitaka Halmashauri za Wilaya na Manispaa nchini kutumia michezo kama nyenzo ya uwekezaji ili kukuza uchumi kwani sekta ya michezo ni kivutio kikubwa ndani na nje ya nchi.

Ulega amesema hayo wakati akihitimisha Tamasha la Ushoroba, Kisarawe lililolenga kuvutia utalii wa wa msitu wa mazingira asilia wa Kazimzumbwi na Hifadhi ya Mwalimu Nyerere.

“Ninatoa wito kwa Wilaya zingine zote kuweza kufanya ubunifu wa namna hii ambayo inachangia kutangaza fursa zilizopo kwenye maeneo yenu, najua mnazo fursa nyingi, zitangazeni kupitia michezo kama ambavyo Kisarawe wamefanya, pia naomba Wadau, wadhamini mbalimbali na mashirika, wanaposikia kuna mazoezi ya namna hii kwenye Wilaya nyingine, sio vibaya kuwaunga mkono” amesema Ulega.

Aidha, Naibu Waziri Ulega amewataka wananchi kuzingatia mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya.