Ajali ya ndege yaua watu 10

0
192

 
Watu kumi wamefariki dunia baada ya ndege ndogo waliyokuwa wakisafiria kuanguka katika jimbo la Jonglei nchini Sudan Kusini.

Ndege hiyo imeanguka katika uwanja wa ndege wa Pieri mara tu baada ya kuruka ikiwa kwenye safari zake za kawaida kutoka jimbo hilo la Jonglei kuelekea mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba.

Katika taarifa yake Waziri wa Uchukuzi wa Sudan Kusini, Madut Biar Yel amesema kuwa, timu ya wataalamu imepelekwa kwenye eneo ilipotokea ajali hiyo kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa awali.

Ndege hiyo inamilikiwa na kampuni ya ndege ya South Supreme ya nchini humo na wakati ajali hiyo inatokea ilikuwa na watu 10 ndani ambao ni abiria na marubani wawili.

Ajali za kuanguka kwa ndege zimekuwa zikitokea mara kwa mara nchini Sudan Kusini, ambapo katika kipindi cha kati ya mwaka 2018 na 2020 ndege 10 zimeanguka katika maeneo mbalimbali nchini humo.