Kituo cha afya Migori kujengwa Nyegere

0
152

Mkuu wa mkoa wa Iringa, – Ally Hapi amemaliza mvutano kuhusu eneo kitakapojengwa kituo cha afya cha Migori wilayani Iringa, na kutoa muda wa miezi minne ili kituo hicho kiwe kimejengwa katika eneo la Nyegere.

Ujenzi wa kituo hicho cha afya cha Migori ni utekelezaji wa ahadi ya Rais John Magufuli aliyoitoa mwaka 2019 akiwa ziarani mkoani Iringa, baada ya Wakazi wa Migori kuomba kujengewa kituo hicho.

Mkuu huyo wa mkoa wa Iringa amelazimika kuingilia kati na kumaliza mgogoro huo ambao umesababisha hali ya kutoelewana baina ya viongozi wa kata ya Migori.