Suu Kyi afunguliwa mashtaka zaidi

0
181

Waendesha mashtaka nchini Myanmar wamemfungulia mashtaka mengine mawili kiongozi wa kiraia nchini humo Aung San Suu Kyi, anayeshikiliwa na jeshi baada ya mapinduzi ya kijeshi.

Raia wa Myanmar wameendelea na maandamano katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo wakipinga mapinduzi hayo ya kijeshi na kutaka Suu Kyi aachiliwe huru, huku jeshi nalo likiendelea kutumia nguvu kutawanya maandamano hayo.

Hadi sasa watu 18 wamefariki dunia nchini Myanmar walipokuwa wakishiriki katika maandamano ya kupinga utawala huo wa kijeshi, baada ya ghasia kuzuka wakati wa maandamano hayo.