Namungo FC mguu ndani Kombe la Shirikisho

0
220

Namungo FC na Primeiro de Agosto (Angola) zimepangwa kwenye Kundi D katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika zikiwa na timu za Raja Club Athletic (Morocco), Pyramids FC (Misri) Nkana FC (Zambia)

Matokeo ya mchezo wa marudiano kati ya Namungo na Primeiro de Agosto ndiyo yatakayoamua timu itakayobaki ndani ya kundi hilo na kuungana na nyingine tatu.

Kwenye mchezo wa kwanza Namungo iliibuka na ushindi wa magoli 6-2 dhidi ya Primeiro de Agosto.

Namungo inahitaji sare au kutofungwa zaidi ya magoli matano ili kuweza kufuzu kuingia hatua ya makundi, wakati Primeiro de Agosto inahitaji ushindi wa magoli matano kwa sifuri ili iweze kufuzu.