BURIANI: Pumzika kwa amani Charity Kasubi

0
226

Mwili wa aliyekuwa Mhandisi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Charity Kasubi umelazwa katika nyumba yake ya milele leo, Februari 17, 2021.

Ibada ya mazishi imefanyika katika Kanisa la City Christian Centre (CCC -TAG) Upanga jijini Dar es Salaam kisha maziko katika Makaburi ya Kunduchi.

Marehemu alizaliwa Juni 30, 1989, aliajiriwa TBC mwaka 2015 na kutekeleza majukumu yake hapo hadi umauti ulipomfika.

Februari 8 mwaka huu Kasubi alipata ajali ya gari wilayani Korogwe iliyopelekea kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) hadi alipofikwa na umauti Februari 13.

Kasubi alikuwa mpole, mkarimu na mnyenyekevu wakati wote. Kasubi ameacha mume na mtoto.

Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina. Inna lillahi wa inna ilayhi raji’un.