Mtandao maarufu wa kurahisisha usafirishaji hasa wa kitalii ujulikanao kama TripAdvisor umetoa orodha ya hifadhi 25 zinazopendwa zaidi duniani zilizoshinda Tuzo za ‘Traveller’s Choice Awards’ huku Tanzania ikiibuka kileleni na pia kuingiza hifadhi tatu katika orodha hiyo.
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti imeshika nafasi ya kwanza kwa kuwa na mandhari yakuvutia pamoja na wanyama wa aina mbalimbali.
Hifadhi nyingine zilizoshinda tuzo hii kutoka Tanzania ni Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro ikishika nafasi ya 12 huku Hifadhi ya Taifa Tarangire yenye kusifika kwa kuwa na Tembo wengi ikishika nafasi ya 14.
Tanzania imekuwa miongoni mwa nchi tatu za Afrika kushinda tuzo hizi huku Kenya ikiwakilishwa na mbuga ya Masai Mara katika nafasi ya tatu na Hifadhi ya Taifa ya Kruger ya Afrika Kusini ikishika nafasi ya tano.