Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Dorothy Gwajima amesema kwa sasa wizara yake haina mpango wa kupokea chanjo ya ugonjwa wa corona, inayoripotiwa kuwepo na kutumiwa na mataifa mengine duniani.
Dkt. Gwajima amejitokeza mbele ya waandishi wa habari jijini Dodoma ili kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa kwa nyakati tofauti kuhusu ugonjwa wa Corona.
“Kwa sasa wizara haina mpango wa kupokea chanjo ya corona (COVIS-19) inayoripotiwa kuwepo na kutumika kwenye mataifa mengine. Ifahamike kuwa serikali kupitia wizara ya afya inazo taratibu zake za kufuata pale inapotaka kupokea bidhaa zozote za afya…,” amesisitiza Dkt. Gwajima.
Aidha, amewahimiza wananchi kufuata njia za kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona zinazoelekezwa na wizara ya afya.
“Tunaendelea kutoa taratibu za kufuata ikiwemo kuimarisha usafi wa mazingira, usafi wa mtu mmoja mmoja, kunawa mikono kwa maji na sabuni, kutumia vipukusi, kujifukiza, kufanya mazoezi mbalimbali, kula lishe bora, kunywa maji ya kutosha bila kusahau matumizi ya tiba asili ambazo taifa hili limejaaliwa,” amesema.
Dkt. Gwajima pia amezitaja baadhi ya bidhaa za tiba asili zinazosaidia kutibu magonjwa mbalimbali ambazo zimehakikiwa na mkemia mkuu wa serikali ikiwemo COVIDOL