DPP afuta mashtaka 183 Kagera

0
176

Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Biswalo Mganga, amefuta mashauri yaliyokuwa yakiwakabili washtakiwa 183 katika mahakama mbalimbali za mkoa wa Kagera.

DPP Mganga amesema ofisi yake imefikia uamuzi huo baada ya kugundua mashauri hayo yamekosa mashiko kisheria.

Mganga ametangaza uamuzi huo mkoani Kagera  wakati akizindua ofisi ya Mwendesha Mashtaka wilayani Karagwe, ambayo imejengwa katika
mji mdogo wa Kayanga.