Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi TBC wapigwa msasa wa kisaikolojia

0
200

Mwanasaikolojia Dkt Chris Mauki akizungumza na Watumishi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambao ni Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi jijini Dar es salaam, ambapo ameelezea namna fikra na mitazamo ya watu inavyoweza kuchochea au kukwamisha mafanikio katika kazi.

Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayub Rioba Chacha akifuatilia mafunzo kutoka kwa Dkt. Chris Mauki

Dkt Mauki ameeleza pia umuhimu wa kuwa na malengo binafsi na kwamba kukosa malengo binafsi au malengo binafsi kutofanikiwa kunakwamisha utendaji kazi wa mtu.

Baadhi ya wafanyakazi wa TBC wakifuatilia mafunzo.

Ameeleza kuwa mtu anapokuwa na malengo ya chini au anapojiona hawezi, fikra na mtazamo huo unachangia kushindwa kutimiza wajibu wake kwa viwango vya juu kwa sababu hatopenda kile anachofanya.

Mhadhiri wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. Chris Mauki akiwafundisha watumishi wa TBC nguvu ya fikra na mtazamo katika utendaji kazi.

Ametumia jukwaa hilo kuwashauri Watumishi hao wa TBC kupanua uelewa wao wa mambo kwani dunia inabadilika, hivyo wasikubali kuwa watu wa kujua kitu kimoja tu katika maisha yao yote.