Mkoa wa Mwanza umezindua zoezi la kuwabaini watoto wenye mahitaji maalum, wa umri wa kati ya miaka minne na sita ili waandikishwe na kuanza darasa la kwanza.
Akizindua zoezi hilo katika kitengo maalum kilichopo shule ya msingi Buhongwa jijini Mwanza, Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza Emmanuel Tutuba amewataka Watendaji wa Serikali za mitaa katika ngazi zote kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa.